Hofu ilitanda kwenye kijiji cha Oleran baada ya jamaa aliyetoweka miaka mingi na kudhaniwa alifariki kurejea ghafla.
Jamaa huyo alifika kijijini humo ambapo jamaa pamoja na mrafiki waliandaa mazishi yake miaka kadhaa iliyopita baada ya kuarifiwa alikuwa amefariki.
Paul Kerich, ambaye jamaa, marafiki na majirani waliamini kuwa aliiaga dunia miaka tatu iliopita alirejea nyumbani siku ya Jumanne na kuzua wasiwasi kijijini.
"Niliskia fununu kwamba watu nyumbani wanaamini nilikufa lakini sikuamini. Nilipofika nyumbani niliona watu wanakusanyika kwangu na mwishowe wakakubaliana mwili waliozika ulikua wa mtu mwingine mbali si mimi," Kerich alisema.
Kerich alidai amekuwa katika shughuli za kikazi miaka hiyo yote.
Jamaa wa familia walisema polisi walipata miili imetupwa mtoni eneo hilo ambapo mmoja ulitambuliwa kimakosa kama wa Kerich.
"Tulipata habari yakwamba kuna watu wawili waliuliwa kwenye mto huo, na kuwa polisi wapeleka miili Narok Hospital mortuary, tukatuma watu wawili uko na wakaupwa ambapo rudisha ripoti kuwa mwili mmoja ni wa Kerich." Jamaa wa familia alisema.