Wakazi wa eneo bunge la Likoni mjini Mombasa wametakiwa kushirikiana kikamilifu na maafisa wa usalama wanaoendesha uchunguzi wa kumsaka mtu aliyeandika barua ya iliyotahadharisha dhidi ya uvamizi katika kanisa moja eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Barua hiyo ambayo inasemekana kuangushwa kwenye lango la kanisa hilo na mtu asiyejulikana inadaiwa kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kujiunga na kundi la Mombasa Republican Council( MRC) na lile la kigaidi la Alshabaab bila kupoteza muda.

Kulingana na mkuu wa polisi wa Likoni Willy Simba barua hiyo ilionekana kuzua hali ya taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo kwamba huenda kukawa na mpango wa kushambulia kanisa hilo.

Aidha Simba anasema kuwa tayari uchunguzi amewaandikia maafisa wa kitengo cha ujasusi (CID) na wale wa kukabiliana na ugaidi (ATPU) ili kutibua mchakato huo.

Hata hivyo Simba amesema huenda ikawa imechangiwa na kutoelewana baina ya viongozi wa kanisa hilo.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka wa elfu mbili kumi na nne kanisa la Joy in Jesusu eneo bunge la Likoni lilivamiwa na genge la majambazi na kupelekea watu watano kuawa huku wengine wakijeruhiwa vibaya.