Generali Edd Ngugi amewahimiza wakenya kukumbatia mradi wa nyumba kumi ili kuimarisha usalama zaidi katika taifa la Kenya.
Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya wakaazi hawajui umuhimu wa mradi wa nyumba kumi na kushindwa kuupa kipaumbele.
Akizungumza siku ya Jumanne katika kijiji cha Mogesa eneo bunge la Bobasi katika sherehe za mazishi ya mwanajeshi mmoja kwa jina Stevine Mokaya aliyeuawa kwenye shambulizi la al-Shababu nchini Somalia.
Generali Ngugi aliomba kila Mkenya kukumbatia mradi wa nyumba kumi ili kuimarisha usalama nchini Kenya.
“Ikiwa mradi huo wa nyumba kumi utaafikiwa hakutakuwa na mashambulizi, vita miongoni mwa mengine ambayo ni mabaya nchini Kenya," alisema Ngugi.
"Himizo langu kwa Wakenya ni kwamba kila mmoja awe mstari wa mbele Kupambana na visa vya uhalifu na kuimarisha usalama zaidi kwa kukumbatia mradi huu,” aliongeza Ngugi.
Aidha Ngugi alisema wanajeshi wa Kenya wataendelea kupambana na al-Shababu nchini Somalia hadi wamalize mashambulizi na uhalifu.
Aidha, alimpongeza marehemu Mokaya kwa kujitolea kupigania Wakenya na kuleta usalama.
Eddi Ngugi alimwakilisha mkuu wa komanda katika mazishi hayo.