Mwenyekiti wa maktaba nchini Samuel Nyangweso amewaomba wakenya kujiunga pamoja kuombea ufisadi unaoendelea kulikumba taifa.
Kulingana naye maombi ndio suluhu kwa ufisadi kwani taifa la Kenya limekuwa likikumbwa na sakata za ufisadi kila wakati.
Akizungumza siku ya jumapili Nyangweso aliomba wakenya kuombea serikali ya kitaifa na zile za kaunti ili taifa la Kenya lisonge mbele kimaendeleo.
“Ufisadi umekuwa ukirudisha taifa letu nyuma sana haswa katika maendeleo naomba wakenya muombee taifa letu ili ufisadi upungue hadi uishe,” alisema Nyangweso.
Aidha, Nyangweso alisema kesi iliyokuwa inamkabili naibu Rais William Ruto na mshtakiwa mweza Joshua Sang katika mahakama ya ICC ilifika kikomo kupitia maombi huku akisema maombi yatafikisha ufisadi katika kikomo.
“Maombi ni suluhisho kwa kila jambo, ufisadi umekuwa ukifanyika katika taifa la kenya kila wakati naomba sisi sote tujiunge kufanya maombi pamoja ili kila kitu kiwe shwari,” aliongeza Nyangweso.
Nyangweso aliomba viongozi wote kutimiza ahadi za maendeleo kwa wakaazi haswa yale waliyoa ahidi wakati wa kampeini.