Mbunge wa Mugirango kusini kaunti ya Kisii Manson Nyamweya amesema wakenya wamepoteza imani kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini na kuomba makamishena wa tume hiyo kuondoka kwa hiari ili wengine kuchaguliwa ambao watasimamia uchaguzi ujao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na mbunge huyo, makamishena wa sasa katika tume hiyo hawastahili kusimamia uchaguzi ujao kwani wakenya hawani imani nao, huku akiomba makamishena wa sasa kujiondoa mapema ili kuruhusu wengine kuchaguliwa.

Akizunguimza siku ya Jumatano usiku katika Redio Citizen kwenye mahojiano, Nyamweya alisema muungano wa CORD utasusia uchaguzi ujao ikiwa makamishena hao hawataondoka kwani hawaaminiki kamwe.

“Ikiwa tunahitaji wakenya kuamini jinsi uchaguzi ujao utafanywa nchini sharti makamishena wa sasa waondoke ili wengine kuchaguliwa upya,” alisema Nyamweya

“Sasa tunahitaji kuokoa wakenya kupitia uchaguzi ujao maana muugano wa CORD uko na mengi ya kufanyia wakenya,” aliongezea Nyamweya

Aidha , aliomba serikali ya Jubilee kutimiza ahadi zake kwani kiongozi huchaguliwa kupitia ahadi za maendeleo na kusema kuzipotimizwa kupitia ahadi ni kukosea wakenya.