Katibu wa wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibichu amewaomba wakenya kuishi kwa amani ili taifa la Kenya kusonga mbele kimaendeleo.
Akiongea hayo siku ya Jumanne mjini Kisii, Kibichu alisema mzozo ukiwa kati ya wakenya, maendeleo hurudi nyuma na kuomba amani kudumishwa kila wakati.
Afisa huyo aliomba wakazi wa kaunti ya Kisii na wa kaunti ya Nyamira kuacha mzozo unaoendelea mpakani Keroka na kusema amani ni msingi wa maendeleo.
Katibu huyo aliwahakikishia machifu kuwa wataendelea kuhudumu kama machifu ata ingawa wanasiasa wanashinikiza kuondolewa na kusema wametambulika na serikali kuu.
“Naomba machifu kufanya kazi yenu sawa sawa na hamtaondolewa kutoka huduma zenu na mmetambulika na serikali ya kitaifa,” alikiri Kibichu.
“Kuwa na mzozo kila wakati unaathiri maendeleo, naomba kila mmoja kuwa na umoja ili taifa letu lisonge mbele,” aliongeza afisa huyo.
Katibu huyo aliwaomba wananchi wote kushirikiana na serikali ya kitaifa na zile za kaunti kuhakikisha maendeleo yamefanywa katika taifa la Kenya.