Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameomba wakenya wote kuishi kwa amani na kuombea viongozi wa taifa la Kenya.
Kulingana na Gavana Ongwae aliyezungumza mjini Kisii, aliomba wakenya kuombea serikali za kaunti na serikali ya kitaifa ili viongozi kuwa na maarifa ya kuongoza na kusongeza taifa hili mbele katika maendeleo kimaendeleo
“Sisi sote ni wakenya hakuna haja ya kugawanya watu kwa misingi ya kikabila naomba sote tuishi kwa upendo na amani,” alisema gavana Ongwae
Pia gavana huyo amehimiza tume huru ya uchaguzi nchini IEBC kuandaa uchaguzi ujao wa mwaka 2017 kwa njia ya haki na uwazi.
Wakati huo huo, Ongwae alisema taifa la Kenya ni taifa ambalo halistahili kurudi katika ghazia zilizozuka mwaka wa 2007/2008 wakati machafuko yalishuhudiwa nchini.
“Naomba uchaguzi ujao wa 2017 uwe wa haki na uwazi ili kila mwanasiasa kuridhika na matokeo ya uchaguzi ujao, naomba sote tupendane kama wakenya na siasa zisije zikatugawa,” alisema Gavana Ongwae.