Wakili mmoja ameondolewa shtaka ya kuharibu mali ya duka kuu la Nakumatt.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Alex Shukran Mwabonje anadaiwa kuvunja troli yenye thamani ya shilingi elfu tano, katika duka kuu la Nakumatt Likoni, mnamo Oktoba 8, mwaka huu.

Mwabonje hata hivyo alikanusha shtaka hilo mbele ya Hakimu mkuu Julius Nange’a siku ya Jumanne.

Mwabonje aliondolewa shtaka hilo baada ya usimamizi wa Nakumatt kuwasilisha ombi la kuondoa kesi hiyo mahakamani.

Mwabonje ni mmoja wa mawakili katika kesi ya wizi wa mabavu inayomkabili mtoto wa Mbunge wa Matuga, Hassan Mwanyoa.