Wakili Vincent Kemosi amejitokeza kuwarahi vijana katika kaunti ya Nyamira kuwachagua viongozi vijana kama njia mojawapo yakubadilisha hali ya uongozi katika kaunti hiyo.
Akiwahutubia wanahabari nyumbani mwake siku ya Ijumaa, Kemosi alisema kuwa yafaa viongozi wachaguliwe wanaoshirikiana na wananchi ili kufanya kazi.
"Kwa muda sasa hatujafanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika eneo bunge la Mugirango Magharibi, na ni jukumu letu sasa kuhakikisha kuwa tunawachagua viongozi walio tayari kufanya kazi pamoja na wananchi," alisema Kemosi.
Kemosi aidha aliongeza kwa kuwarahi vijana kuwachagua viongozi vijana kwenye nyadhifa mbalimbali mwakani huku pia akiwahimiza wananchi kukumbatia amani.
"Ombi langu kwa vijana ni kuwachagua vijana kwenye nyadhifa za kisiasa kwa maana tuna vijana wengi ambao wamesoma na wana nia safi ya kuwafanyia wananchi kazi, ila ni ombi langu kwao kukumbatia amani," aliongezea Kemosi.