Wakili Steven Mogaka amewasuta viongozi ambao hutumia barabara ya Kebirigo-Mosobeti-Metamaywa kama kigezo cha kujinufaisha kisiasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

"Barabara (kebirigo-Mosobeti-metamaywa) hii imekuwa ikitumiwa kama kitega kura kwa kuwa kila mwanasiasa akija husema kwamba barabara hii itategezwa ilhali hahitegezwi," alisema Mogaka.

Barabara hiyo imekuwa itengenezwe kutoka serikali ya Moi lakini hadi kwa sasa haijatengenezwa.

Hivi majuzi, Rais Uhuru Kenyatta aliifungua rasmi kutengenezwa vile Moi alifanya akiwa uongozini, na vile vile Rais Mwai Kibaki alifanya vivyo hivo kuifikisha miaka thelathini tangu itajwe kutengenezwa. 

Sasa wakili amewaomba viongozi kutoitumia kila mwaka barabara hiyo haijatengewa pesa kwa kuwa imepiwa kiboko cha kutengenezwa.

"Nawaomba wanasiasa na viongozi kutoitumia barabara hiyo kwa kuwa kila mwaka hahitengewi fedha za kuikarabati kwa kuwa yasemekana imetengenezwa," aalisema Mogaka aliyekuwa akiyasema siku ya Jumapili katika mji wa Nyamira.