Wakili mmoja amefikishwa kizimbani katika mahakama ya Mombasa kwa kosa la kughushi hati ya kiapo.
ADVERTISEMENT
Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!
Aprili 8, 2008, wakili Samuel Odhiambo anadaiwa kughushi hati ya kiapo ya Daniel Njuguna Kibeti kwenye kesi inayoendelea mahakamani.
Samuel amekanusha madai hayo mbele ya hakimu Diana Mochache na kutozwa dhamana ya shilingi laki moja ama pesa taslimu shilingi 50,000.
Kesi hiyo itasikilizwa Septemba 19, 2016.