Wakili mmoja jijini Mombasa amefikishwa kizimbani kujibu shtaka la kuvunja troli ya mizigo, iliyokuwa mali ya duka kuu la Nakumatt.
Alex Shukran Mwabonje andaiwa kuvunja troli hiyo yenye thamani ya shilingi elfu tano, katika duka kuu la Nakumatt Likoni, mnamo Oktoba 8, mwaka huu.
Mwabonje alikanusha shtaka hilo mbele ya Hakimu mkuu Julius Nange’a siku ya Jumanne.
Kesi hiyo itaendelea leo (Jumatano) baada ya usimamizi wa Nakumatt kutaka kufanya kesi hiyo nje ya mahakama.
Mwabonje ni mmoja wa mawakili katika kesi ya wizi wa mabavu inayomkabili mtoto wa mbunge wa Matuga, Hassan Mwanyoa.