Aliyekuwa mwenyekiti wa LSK kanda ya Bonde la Ufa Wakili Bernard Kipkoech Ng'etich amepinga hatua ya wabunge kutaka kuongeza muda wa Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakili Ng'etich alisema kuwa kwa mujibu wa katiba, bunge halina mamlaka hayo.

"Kile ambacho nafahamu ni kwamba Wabunge hawana mamlaka kuongeza muda wa IEBC labda tufanyie katiba marekebisho," Ng'etich alisema.

Wakati huo huo, Ng'etich ametoa wito kwa jamii humu nchini kukumbatia wanawake katika maswala ya uongozi.

Kwa mujibu wake, kumekuwa na kasumba ya wanawake kuteuliwa badala ya kuchaguliwa na mpiga kura, swala ambalo alisema linafaa kukomeshwa.

"Nafikiri wakati umefika jamii ianze kuwachagua wanawake katika nyadhifa mbali mbali," alisema.