Wakimbizi wa ndani katika kaunti ya Kisii wameiomba serikali kutojiondoa katika mkataba wa Roma.
Hii ni baada ya baadhi ya maafisa wakuu serikalini wakiwemo wabunge kupendekeza kuwa Kenya inastahili kujibandua kutokana na mkataba huo.
Kulingana na wakimbizi hao ikiwa taifa la Kenya litajiondoa kutoka mahakama ya ICC viongozi watakuwa na nafasi kubwa ya kutekeleza uhalifu bila kujali kwani hakuna mahakama itakayo wahukumu wakisema ICC uwapa tumbo joto kali wahalifu wa kivita hivyo basi huzuia ghasia kutoibuka.
Wakizungumza mjini Kisii wakimbizi hao wa ndani kwa ndani wakiongozwa na David Mokaya na Dismas Nyakundi waliomba Kenya kusalia kuwa mwanachama wa mahakama ya ICC.
“Vile kesi za baadhi ya wakenya zimekuwa katika mahakama ya ICC wengi wamejifundisha kutofanya uhalifu lakini sasa tukiondoka wengi watahusika katika ghasia kwani hakuna mahakama itawahukumia maana hapa Kenya hawatakuwa na uoga mkubwa kama ICC,” alisema Mokaya.
Aidha, wakimbizi hao waliokosoa maombi yaliyofanyika katika uwanja wa Afuraha katika kaunti ya Nakuru kwa kutowafidia.