Wakongwe kutoka kaunti ya Kisii wametaka serikali kuu kutafuta njia mwafaka kuwalipa pesa za msaada ambazo wanapokea kila baada ya miezi miwili.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongea na mwandishi huyu siku ya Jumanne katika uwanja wa Gusii walipokuwa wamekutana kupokea pesa hizo waliiomba serilikali kuwatumia peasa hizo kupitia kwa simu zao.

 Samuel Mose, mmoja wa waliongea na mwandishi huyu, alisikitika na jinsi ambavyo wengi wa wakongwe wana sumbuka wanapo ziendea pesa hizo.

"Mzee kama mimi nina miaka 71 naumwa na miguu. Naona iwe vizuri watutumie kupitia mpesa kwa vile nina simu na nimejiandikisha na Safaricom," alishauri Mose.

Bosire Makambi ambaye alionekana mkongwe zaidi alikuwa tayari ashaanza kurudi nyumbani ambapo alisema kuwa itabidi serikali itafute njia nzuri ya kuwapokeza pesa hizo. 

"Mimi naomba wanaosimamia kutujali sisi. Hatuna nguvu ya kutembea safari ndefu. Huenda nisije hapa tena, nitamwacha mjukuu wangu ambaye tulikuja naye apewe aniletee,” alisema Bosire. 

Serikali kuu huwapa pesa wakongwe na mayatima ili kuwasaidia kujikimu kimaisha.