Wakongwe na mayati waliokuwa wanasubiri kulipwa pesa zao katika uwanja wa Gusii walighadhabishwa kutokana na pesa hizo kukosekana, na kuambiwa wasubiri hadi tarehe 29 mwezi huu.
Wakiongea siku ya Jumanne na mwandishi huyu, wakongwe hao na mayatima walisema kuwa wameghadhabishwa sana na jinsi shughuli hiyo ilivyoandaliwa na pesa zao kukosekana.
Baadhi ya waliongea walisema kuwa matarajio ya kupokea pesa hizo, hasa mayatima, yalikuwa yana msaada kubwa kwa kuwa wangezaidika kulipa karo kwa kuwa wanafunzi wengi wanaendelea na shughli za kurudi shuleni.
Wakongwe nao, hasa wa miaka, 60 kuenda juu walisema kuwa walikopesha pesa, na kukosekana kwa pesa hizo litakua jambo baya kwao.
“Niliitarajia kupata hizo kwa kuwa zingenizaidia hasa kulipa karo ya shule kwa ndugu zangu lakini kwa sasa tumeambiwa kuwa hadi tarehe 29 jambo ambalo sikufurahishwa nalo,” alihoji Denis Kiage, mmoja wa mayatima wanaonufaika na mradi huo.
“Tumepigwa na jua tangu asubuhi na njaa pia na sasa sina pesa hata ya kununua soda au maji kwa kuwa kile nilichiokuwa natarajia sikupata,” alisema mzee Mokaya wa Miaka kumi 72.
Aidha, wameiomba serikali kuu kuweka mikakati kabambe hasa wakati wanatoa pesa hizo.
Kulingana na wasimamizi wa benki ya KCB, mtandao wao ndio uliwafeli, jambo lililowapelekea kuhairisha hadi talehe 29 mwezi huu, huku akiwaomba watu wote kuwa na subira kwa kuwa mambo yao yatarekebishwa na kuwa shwari.