Wakongwe na mayatima kutoka Wadi ya Kisii ya Kati, eneo Bunge la Nyaribari Chache wamefurahia hatua ya Serikali kwa kuamisha pesa zile wanawapongeza hadi kwenye benki kama njia moja ya kuleta uwazi wakati wanagawiwa pesa hizo.
Wakiongea na Waandishi wa Habari siku ya Jumapili katika sehemu ya Nyanchwa, Kaunti ya Kisii, baadhi ya wakaazi hao walipongeza Serikali Kuu kwa kuchukua hatua hiyo kwa kuwa wanatarajia kuwa hiyo ni njia moja ya kuleta uwazi na kukomesha wale waliokuwa wanapata ‘sabuni’ kutoka kwa pesa hizo na kusema sasa siku zao zimeisha.
“Serikali imefanya jambo la busara kwa kuwa hapo awali wengi wetu tulikuwa hatupati pesa hizo kama ipasavyo hata kama zilikuwa zinatolewa, lakini kwa sasa tuna matumaini kuwa tutapata hizo kupitia benki bila yeyote kuleta ufisadi,” alihoji Bosibori Mokaya, mkaazi wa eneo hilo.
Wakongwe na mayatima hao kwa sasa watakuwa wanapokea pesa hizo kupitia benki ya Kenya Commercial Bank (KCB) hii ni njia moja ya kuepuka na mizozo ya kila mara kwa kuwa kulikuwa na tetesi ya watu kutopata pesa hizo pamoja na madai kuwa kuna wenye walikuwa wanachukua pesa hizo na kujifaidi wenyewe bila kuwajali wakongwe hao na mayatima.
Hapo awali walikuwa wanapatiwa pesa hizo katika vituo vya Posta na walikuwa wanajulishwa na Machifu wao ambapo wengi wamesema wakati mwingine hata Machifu walikuwa wananyamazia ujumbe huo bila kuwapasha.
Kwa sasa wakongwe hao wamepewa kadi kutoka Benki ya KCB ambayo wataitumia kupokea pesa hizo baada ya kila miezi mitatu.
Kulingana na James Basueti mmoja wa mayatima ambaye anafaidika na mradi huo, kadi hiyo itawasaidia kuleta uwazi nakupokea pesa hizo ili kijiendeleza kimaisha.
Aidha, wamewakashifu watu wengine ambao hujiandikisha kuwa ni mayatima ilhali wana wazazi kitendo alichokisema kuwa hiyo ni kujitakia mabaya.