Wakulima wa majani chai katika Kaunti ya Kisumu kwenye maeneo yanayopakana na Kaunti ya Kericho wameshauriwa kuuzia kampuni ya chai ya Kericho mazao yao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakulima hao kutoka eneo la Awasi kwenye Kaunti ya kisumu wametakiwa kupanua na kuboresha kilimo hicho kwa kupeleka mazao yao kwenye kampuni hiyo ambapo watalipwa vizuri na kwa wakati.

Mwanasiasa, Florence Ong'udi, ambaye anawania kiti cha uwakilishi wa Wadi ya Angoro Kaskazini alisema kuwa wakulima hao wananyanyaswa na 'mabrocker' wa chai ambao huchukua bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima wakiahidi kuwalipa pesa na baadaye hutoroka.

Mwanasiasa huyo alisema hayo wakati alipokutana na baadhi ya wakulima wa majani chai kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa katika kituo cha kuuza cha Angoro, siku ya Jumanne.

“Nimeona mna nia ya kuimarisha kilomo cha chai katika eneo hili lakini bado mnasongwa na changamoto za watapeli,” alisema Ong'udi.

Aidha, Ong'udi aliahidi kuwasaidia wakulima hao wachanga kutoka ene hilo kupeleka majani yao wenyewe katika kampuni ya Kericho na kusaidia kupanua kilimo hicho katika eneo hilo.