Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amesema wakaazi wa kaunti hiyo wataanza kupata mafunzo ya jinsi watatumia ‘Green House’ ili kujiendeleza katika kilimo na kiuchumi.
Ongwae alikiri kuwa wakaazi wa kaunti yake watapata mafunzo jinsi ya kutumia ‘green house’ hivi karibuni ili wakaazi wawe wakifanya kilimo yao kwa njia ya kuzalisha matunda.
“Nitahakikisha kuwa wakaazi wa kaunti yangu mumefundishwa jinsi kilimo hufanywa kwa ‘ green house’ na jinsi inatumika ili mfanye kilimo bila kusumbuliwa na jua kali na hata wakati wa mvua hunyesha kwa wingi ambayo hualibu mazao yenu,” alisema Ongwae.
Viongonzi waliohudhulia sherehe hiyo mbunge wa Nyaribari Chache Richard Tong’i naibu gavana wa kaunti ya Kisii joash Maangi waliunga mkono hatua ya gavana ongwae kwa kueneza kilimo kwa kila upande baada ya kukiri kuwa wananchi kupokezwa mafunzo hayo ya kutumia ‘Green House’ ili waweze kujiendeleza katika kilimo na kibiashara
Wananchi walionekana kufurahishwa na matamshi ya gavana ongwae na kusema hiyo ndio njia moja ya kuhakikisha kilimo kimeimarishwa katika kaunti ya kisii
“Vile Ongwae amesema kuwa tutafundishwa jinsi ya kutumia Green house tunaomba pia aweze kutununulia hizo green house ili tusiwe tunajua jinsi ya kutumia hiyo ‘green house’ na hatuna katika nyumba zetu,’ alihoji peter Maganga mkaazi.