Wakulima wa majani chai kutoka Wadi ya Gesima, Kaunti ya Nyamira waliotoa hekari nane zitakazotumika kwa ujenzi wa kiwanda kipya cha kusaga majani chai, wamesema wako tayari kuhakikisha ujenzi huo umekamilika.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea mmoja wa wakulima hao Yabesh Mokaya katika shamba lake sehemu ya Matunwa, amesema hiyo ni njia moja ya kuleta maendeleo katika eneo hilo.

“Kiwanda hicho kikijengwa kitaleta maendeleo hasa kwa vijana wetu maanake bila shaka watapata ajira,” alisema Mokaya.

Aidha, alisema changamoto zinazowakumba wakulima wa majani chai wanapopeleka majani chai yao kwa nyumba ya kununua (buying center] hupata hasara baada ya majani chai hayo kukauka kwa kutochukuliwa kwa wakati ufahao.  

Kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Matunwa Wadi ya Gesima. Hii ni baada ya makubaliona kati ya wasimamizi wa wakulima wa kiwanda cha Nyansiongo na serikali ya Kaunti ya Nyamira.

Wakulima hao kwa jumula wamekuwa wakikatwa Sh3 kwa kila kilo kwa takiribani miaka mitatu na kufikisha Sh143 milioni pesa ambazo zitagaramia ujenzi huo.

Kwingineko wakulima hao wanakadiria hasara  kubwa kutokana na kiangazi  ambacho kimekua kimewasumbua kwa muda mrefu tangu Disemba mwaka jana na kusababisha kukauka kwa mmea huo wa majani chai ukiwa shambani