Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima wa majani chai kutoka eneo bunge la kitutu Chache kaskazini kaunti ya kisii wameomba viwanda vya kusaga majani chai kuwa chini ya uongonzi wa serikali za kaunti.

Hii ni baada ya wakulima hao kusema kuwa halmashauri inayosimamia sekta hiyo kwa sasa imeshindwa kutekeleza kazi yao kikamilifu, haswa jambo la kukaa kwa majani chai katika vituoni kwa mda mrefu bila kupimwa, na kukosa kujenga viwanda katika kila kaunti na mengine.

Wakizunguza na waandishi wa habari siku ya Alhamisi katika wilaya ya Marani, wakulima hao wakiongozwa na Zachary Otwoma mmoja wa wawakilishi waliomba sekta ya majani chai kuwa chini ya serikali za kaunti ili kushughulikiwa kikamilifu jinsi wanavyohitaji.

“Majani chai yakiwa chini ya serikali za kauti hatutakuwa na changamoto nyingi haswa majani chai yetu kukaa katika vituoni kwa zaidi ya siku tatu bila kupimwa uzani na kutochukuliwa kwa mda usiofaa,” aldokeza Douglas Nyaanga, mkulima.

“Serikali ya kaunti iko na uwezo wa kujenga viwanda vya kupima majani chai ikilinganishwa na KTDA ambayo inaendelea kutusababishia hasara,” aliohoji Charles Obiri, mkulima mwingine.

Ombi hilo limebaki bila jibu halisi, huku likisubiriwa kushughulikiwa upesi kwani wakulima hao wamesema itakuwa vyema zaidi serikali za kaunti zikisimamia sekta ya majani chai.