Wakulima wa majani chai kutoka eneo bunge la Borabu kaunti ya Nyamira wametishia kutochukuwa majani chai yao katika kituo cha ununuzi cha Gucha ikiwa hawatahudumiwa vyema.
Hii ni baada ya makarani wa kupima majani chai katika kituo hicho kususia kuenda kupima majani chai hayo kwa siku nne mfululizo tangu siku ya Jumatatu wiki hii.
Wakiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano wakulima walidikeza kuwa ni ufisadi unaendelea kufanywa dhidi yao huku wakiwaomba wakurugenzi wa kiwanda cha Kebirigo kuchukuwa hatua ya haraka kwa kuwatuma makarani kupima machani chai hayo la sivyo wang’oe miti ya mumea huo katiaka mashamba yao.
‘’Tulileta majani chai siku ya Jumatatu katika kituo hiki cha Gucha na leo yameungua hatujawai mwona karani wa kupima uzani hata mmoja akija kupima majani chai yetu tumepata hasara tayari na majani chai mengine yangali kwenye mashamba yetu yakiaribika tufanye nini?’’auliza Enock Momanyi mkulima wa majani chai katika kituo cha Gucha.
‘’Tunahitaji neno la mwisho kutoka kwa wakurugenzi wa kiwanda cha Kebirigo kama hawataki majani chai yetu tung’oe mmea katika mashamba yetu lazima tutendewe haki kama wakulima,’’ alisema Jeremiah Onsongo mkulima.
Hii si mara ya kwanza wakulima hao kulalamikia kutochukuliwa kwa majani chai yao na hata kupimwa uzani jambo ambalo wanalalamikia kila mara na kuendelea kupata hasara.