Wakulima wa pareto katika eneo la Nakuru wameitaka serikali kutambua kilimo cha zao hilo jinsi inavyotambua kilimo kingine.
Wakiongea katika hafla ya mafunzo ya pareto katika eneo la Kuresoi siku ya Ijumaa, wakulima hao walisema kuwa serikali kuu imepiga jeki kilimo cha miwa, mahindi na miraa huku ikitelekeza wakulima wa pareto.
Kwa sasa wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuwa na ujumbe mwafaka kwa wakulima wakati wa ziara yake mjini Nakuru mwezi Juni.
Hata hivyo wamesema kuwa wana matumaini ya kuimarisha kilimo chao kwa ushirikino na serikli ya jimbo la nakuru ambayo wametaja kuwa imewapa msaada wa aina yake.
MCA wa Nyota Njoroge Gichamu amesema kuwa “Serikali ya jimbo la Nakuru imetoa mamilioni ya mbegu za pareto katika maeneo ya Bahati, Kuresoi, Naivasha Subukia na maeneo mengine mengi.”
Wakati uo huo Gichamu ameitaka serikaki hiyo kutenga hela za kutosha zitakazoweza kukimu kilimo hicho katika jimbo la Nakuru akikitaja kama kitakachochangia pakubwa kuimarisha uchumi wa kaunti ya Nakuru na taifa kwa jumla.