Wakulima katika kaunti ya Nyamira wanafurahia kazi ya mikono yao kwa kuwa mimea yao imenawiri vizuri shambani. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima hao kutoka kaunti hiyo wanafurahia kuwa mimea yao shambani hasa mahindi yamenawiri na kustawi vizuri mwaka kuliko miaka mingine iliyopita.

Matokeo hayo yamejiri baada ya wakulima hao kupata mafunzo kem kem kutokana na mpango uliofanywa na afisa mkuu wa kilimo katika kaunti hiyo.

Wakulima hao pia wamesema kuwa mwaka huu ugonjwa wa mahindi uliojitokeza mwaka uliopita na kuharibu mimea nyingi shambani haujaonekana msimu huu.

"Msimu huu tumeona dalili kuwa mimea yetu itatupa mapato mazuri kwa sababu hatujakumbana na janga lolote shambani," alisema Mosota, ambaye ni mkulima. 

Afisa huyo wa kilimo alisema kuwa bado ana mpango wa kuleta wataalamu wa kilimo ambao watawaelimisha wakulima hili kuhakikisa kuwa hali ya mapato inaongeza hili kukabiliana na janga la njaa katika kaunti hiyo.

"Ninao mpango kuwaleta wataalamu wa kilimo watakao wapa mafunzo katika kaunti yetu," alisema afisa huyo.