Wakulima katika kaunti ya Nakuru wamehimizwa kukumbatia teknolojia mpya kuimarisha kilimo.
Akizungumza Jumanne katika kaunti ndogo ya Njoro wakati wa maonyesho ya kilimo eneo hilo, afisa mpanga hafla hiyo Julie Wanjiru Chege alisema kuwa kilimo cha teknolojia ni muhimu sana na wakulima wanafaa kukumbatia kilimo hicho ili kuimarisha mazao.
Isitoshe alitoa wito kwa wakulima kuchukulia kwa uzito hafla za maonyesho ya kilimo ili wapate maarifa.
"Ningetoa wito kwa wakulima kuhakikisha kwamba wanachukulia kwa uzito mafunzo ya maarifa kuhusu kilimo," Jullie alisema.
Wakati huo huo alitoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba wakulima wanapigwa jeki hata mashinani.