Share news tips with us here at Hivisasa

Mwaakilishi wa wakulima katika kanda ya Nakuru Kaskazini ameitaka kaunti ya Nakuru kuimarisha shuguli za ukulima.

Bwana Joe Maina alisema jana katika kituo cha kibiashara cha Bahati kwamba kaunti haina budi kuimarisha juhudi za ukulima.

"Tunataka Kaunti ya Nakuru kuwekeza mikakati bora ambayo itasaidia kuimarisha juhudi za uzalizaji wa chakula,” alisema Maina.

Alisema kuna haja juhudi za kuimarisha maziwa zipigwe jeki.

"Ufugaji wa ng'ombe za maziwa unastahili kuboleswa kwa minajili ya utoaji wa maziwa,” alisema Maina.

Pia Maina alisema kwamba kuna haja ya kaunti kuwapa wakulima mafunzo ambayo yatawasaidia kuimarisha uzalizaji wa maziwa.

"Wakulima wanapaswa kupokea mafunzo ili wawe katika hali nzuri ya kuimarisha ufugaji bora,” alisema Maina.

Maina aliendelea kusema kwamba kaunti inapaswa kutenga kiasi cha hela kwa manufaa ya wakulima.

"Juhudi za ukulima hapa Nakuru Kaskazini zinalemezwa na ufungufu wa senti na tunataka kaunti inongeze hela zaidi kwa wakulima,” alisema Maina.

Hata hivyo Maina aliwambia wakulima wasitegemee kaunti kwa kila kitu bali watafute senti kwingineko kwa minajili ya kuimarisha ukulima.