Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mashirika ya kijamii katika eneo la Magharibi mwa nchi, yametakiwa kuwa katika mstari wa mbele kushughulikia mahitaji ya wananchi.

Afisa mpanga ratiba katika shirika la KMET Sam Owoko, amewashtumu baadhi ya wakuu wa mashirika ya kijami, anaosema lengo lao ni kupata pesa kutoka kwa wafadhili kisha kukosa kuwasaidia wananchi.

''Kuna tetesi kuwa mashirika ya kijamii hatuzungumzii masuala kuhusiana na rushwa ilhali ndilo jukumu letu kuzungumzia maswala yanayomhusu mwananchi," alisema Owoko.

Amesema baadhi ya wanaharakati huhongwa na maafisa wa serikali za kaunti, ili kutozungumzia visa vya ufisadi vinavyoripotiwa kwenye serikali za kaunti.