Kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohamed Maalim amewaonywa walanguzi wa mihadharati dhidi ya kuendeleza biashara hizo katika kaunti ya Mombasa.
Maalim alisema kuwa serikali iko imara katika kupiga vita ulanguzi wa dawa za kulevya kote nchini, na kuitaja biashara hiyo kuwa imekithiri sana eneo la Mombasa na kususitiza kuwa kamwe hatalegeza kamba kuwakabili walanguzi wakuu.
Aidha, ameitaka halmashauri ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati nchini NACADA kujitahidi kuwasilisha huduma zake katika kaunti hii.
Maalim ameeleza kusikitishwa kwake na ongezeko la idadi ya waathiriwa wa mihadarati, akisema wengi hawana uwezo wa kujiunga na vituo vya kurekebisha tabia vya kibinafsi kutokana na gharama ya juu ya malipo.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake, afisa huyo amelitaka shirika hilo kujizatiti kuhakikisha waathiriwa wa mihadarati katika kaunti hii wananufaika na huduma za shirika hilo.