Imebainika kuwa jamii ya walemavu eneo la Pwani na taifa kwa jumla bado hawana la kujivunia licha ya katiba kutoa fursa kwa jamii hiyo kupata nafasi za uwakilishi katika nyadhfa mbali mbali serikalini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kauli hii ilitolewa na mshirikishi wa shirika la walevamu kanda ya Pwani Hamisa Maalim Zaja siku ya Ijumaa alipokuwa akizungumza namwanahabari huyu.

Aliongeza kuwa walemavu wa kike wakisalia kutengwa katika uwakilishi kote nchini.

Aidha, bado bunge la kitaifa na mabunge ya kaunti hayajapitisha sheria zinazofaidi jamii hiyo hivyo basi kuchangia walemavu wengi kutaabika kimaisha.

Pia ametaka walemavu kuteuliwa katika nyadhifa mbali mbali serikalini.