Jamii ya walemavu katika Kaunti ya Mombasa imelalamikia jinsi zabuni zinavyotolewa kwa ubaguzi katika kaunti hiyo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa kundi la vijana la Al-iman mjini Mombasa Abdallah Abubakar, amesema kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa imeshindwa kuzingatia mgao wa asilimia 30 ya zabuni za kaunti kwa makundi ya akina mama, vijana na walemavu.

Naye mwanaharakati wa wanawake katika eneo la Nyali Jamilla Hassan amesema kwamba ni bayana zabuni hizo zimekuwa zikitolewa katika njia ya ubaguzi huku wanawake, vijana na walemavu wakipuuzwa.

Jamilla ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kumuangazia mwanamke wa mashinani ili anufaike na zabuni hizo na kupanua shughuli zake za kibiashara na wala sio kuwaangazia wanawake waliyobobea katika maswala ya kibiashara na ambao wameajiriwa.

"Tunaiomba serikali ya kaunti ya Mombasa kuhakikisha kuwa inawaangazia walemavu na kuwasaidia zaidi katika maswala ya kimaendeleo kwa kuwapa zabuni ili kujiendeleza kimaisha," alisema Jamilla wakati wa mkutano na jamii ya walemavu mjini Mombasa siku ya Jumatatu.