Mrundiko wa vitambulisho. Jamii ya walemavu Mombasa imeitaka serikali kuhakikisha vitambulisho vyao vinatolewa kwa haraka. Picha/ nation.co.ke
Idara ya usajili wa watu Kaunti ya Mombasa imehimizwa kulipa kipau mbele swala la utoaji vitambulisho kwa jamii ya watu wanaoishi na ulemavu.
Kauli hii imetolewa na mwenyekiti wa muungano wa walemavu eneo bunge la Jomvu, Hamis Rajab, aliyesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaoishi na ulemavu Mombasa hawana vitambulisho.Rajab aidha alisema kwamba anastaajabishwa na jinsi vitambulisho vya watu wanaoishi na ulemavu vinakawia kutolewa, jambo alilolitaja kuvunja moyo miongoni mwao.Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumanne, Rajab alisema kukosekana kwa vitambulisho miongoni mwa walemavu kumechangia kushudiwa kwa changamoto mbalimbali za kimaisha wanazopitia.Mwenyekiti huyo amesema kuwa jamii ya walemavu ina haki kikatiba ya kupata vitambulisho, kwani stakabathi hizo muhimu ndizo zitakazo wawezesha kuchagua viongozi wanaojali matakwa yao.