Kinara wa Nasa Raila Odinga na raisi Uhuru Kenyatta. [diasporamessenger.com]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Baadhi ya walemavu kaunti ya Mombasa wamemtaka raisi Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga kufanya mazungumzo ili kutatua mgogoro wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini kwa sasa.

Wakiongozwa na Stephen Mutinda ambaye ni mlemavu wa kuona anasema kuwa iwapo Jubilee na Nasa hazitaelewana  basi huenda taifa likajipata lwenye machafuko kama yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumapili Mutinda alisema kuwa walemavu ndio wanaoathirika zaidi wakati kunapozuka machafuko nchini.

Mutinda amewataka vinara wa Nasa kufutilia mbali mpango wao wa kumuapisha kinara wao Raila Odinga na kalonzo Musyoka Januari 30,2018, akisema kuwa hatua hiyo huenda ikasababisha vita nchini.

Kauli hii inajiri baada ya Nasa kusisitiza kuendelea na mpango wao wa kuwaapisha vinara wao ili wawe viongozi wa mabunge ya wananchi.

Itakumbukwa kuwa rais Uhuru Kenyatta amenukuliwa mara nyingi akisema hatashiriki mazungumzo ya kisiasa na mrengo wa NASA kwa kuwa msimu wa siasa umeisha huku upande wa NASA ukisisitiza kuwa  utamuapisha Raila na Kalonzo kama rais na naibu wake.