Walemavu eneo la Pwani wameitaka serikali pamoja na upinzani kuhakikisha uchaguzi ujao hautakumbwa na machafuko kama yale ya mwaka 2007/2008.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Bakari Mwakilesho, mwakilishi wa jamii ya wanaoishi na ulemavu eneo la Chigombero, huko Lunga Lunga, amesema ghasia za kisiasa huathiri pakubwa walemavu, ikizingatiwa hawana uwezo wa kujitetea.

Mwakilesho amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha uchaguzi huo ni wa huru na amani, ili kulinda usalama wa walemavu.

Haya yanajiri baada ya kubainika kuwa zaidi ya watu elfu moja kati ya idadi ya waliouawa katika ghasia za uchaguzi wa mwaka 2007/2008 walikuwa walemavu.

Mwakilesho ameitaka Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, kuhakikisha vituo vya kupiga kura viko salama kwa walemavu.

“Tunataka vituo vya kura kulindwa ili walemavu wasidhulumiwe,” alisema Mwakilesho.

Aidha, ametaka walemavu kupewa kipaumbele na nafasi za kwanza wakati wa shughuli hiyo ya kupiga kura.