Mwakilishi wa walio na ulemavu katika bunge la kaunti ya Nakuru Emmah Mbugua ametoa wito kwa serikali kutenga nafasi zaidi za uongozi kwa watu walio na ulemavu katika jamii.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na mwandishi huyu mjini Nakuru Jumatatu , Emmah Mbugua ambaye pia ni mwakilishi mteule wa eneo mbunge la Bahati aliteta kuwa asilimia tano ambayo imetengwa kikatiba kutoa nafasi za uongozi kwa walio na ulemavu haitoshi.

Kwa muujibu wake, asilimia hiyo inamaana kuwa ni mwanamke na mwanamme mmoja pekee ambao watapata nafasi ya kuwakilisha walio na ulemavu katika kaunti ya Nakuru, idadi ambayo ametaja kama iliyo ndogo sana.

Kando na hayo, Mbugua aliashiria kuwa idadi ya walio na ulamavu katika bunge la seneti pia iko chini, hali ambayo alisema haiwapi nafasi ya kuchangia.