Zaidi ya walimu elfu kumi watapandishwa vyeo mwaka huu ili kuimarisha viwango vya elimu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubia kongamano la walimu wakuu wa shule za msingi mjini Mombasa siku ya Jumatano, afisa mkuu wa Tume ya TSC Nancy Macharia amesema serikali imetenga shilingi bilioni mbili ili kufanikisha zoezi hilo.

Ameongeza kuwa nafasi hizo za walimu wa shule za msingi na walimu wakuu zitatangazwa hivi karibuni.

Aidha, Bi Macharia amepuzilia mbali madai kuwa zoezi hilo lina ufisadi ndani yake na kusema kuwa walimu waliofuzu kupandishwa madaraka pekee ndio watafanikiwa katika zoezi hilo.

Macharia pia ametoa wito kwa wazazi kushirikiana na walimu ili kuhakikisha kuwa utovu wa nidhamu shuleni ni jambo ambalo linazikwa katika kaburi la sahau.