Imebainika kwamba wengi wa walimu kutoka Kaunti ya Kisumu wanajiunga na chama cha kutetea maslahi ya walimu cha Knut.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na katibu mkuu wa Knut tawi la Nyando Ephraim Kananga.

Akizungumza na wanahabari katika afisi yake iliyoko Awasi, kananga alisema hatua hiyo imechangiwa zaidi na huduma za Knut kwa wanachama wake.

“Ripoti amabazo tunaendelea kupata kutoka zoni mbali mbali katika Kaunti ya Kisumu zinaashiria kwamba walimu wengi wanajiunga na chama cha Knut. Baadhi ya walimu wanahama kutoka chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na taasisi za masomo ya juu Kuppet,” alisema Kananga.

Aidha, alisema kuwa kama chama, wataendelea kusimama dhabiti kuhakikisha maslahi ya wanachama wao yanaangaliwa vyema na kuzingatiwa na serikali.

“Naweza nikasema hatua ya walimu kujiunga na chama chetu kinatokana na msimamo wa chama hichi kujitolelea kudumisha umoja wa walimu wa taifa hili na vile vile kupigania mahitaji ya wanachama wake kwa dhati,” alisema Kananga.