Walimu kutoka kaunti ndogo ya Masaba Kaskazini wameapa kuandamana hadi kwenye afisi za tume ya kuajiri walimu TSC, jijjni Nairobi, kulalamikia kutolipwa kwa mishahara yao ya mwezi wa Septemba.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika shule ya msingi ya Nyakongo siku ya Jumatatu, wakati wa sherehe zakuwaombea wanafunzi wa darasa la nane, Naibu katibu wa chama cha KNUT tawi la Masaba Kaskazini Bw James Oteki alisema kuwa wamekuwa wakingoja kulipwa pesa zao hali iliyo walazimu kupanga safari ya kufika kwenye afisi kuu za TSC mwishoni mwa mwezi huu.

"Walimu wa eneo hili wamekuwa wakingoja kwa muda kulipwa mishahara yao na sasa imetulazimu kupanga safari yakuwasilisha malalamishi yetu kwa afisi za TSC mwishoni mwa mwezi huu,” alisema Oteki.

Katibu huyo aidha alisema kuwa walimu wengi wamekuwa na changamoto za ukosefu wa pesa hali ambayo imeathiri shughuli zao za kila siku huku wengine wakishindwa kulipa mikopo ya benki.

"Kwa sasa walimu wamekumbwa na changamoto za ukosefu wa fedha hali ambayo imeathiri shughuli zao za kawaida huku wengine wakishindwa hata kulipia mikopo ya benki mbalimbali,” alisema Oteki.

Katibu huyo alisema kuwa chama cha walimu kwenye tawi hilo la Masaba Kaskazini ki tayari kuwalipia walimu nauli itakayo wawezesha kufika jijini Nairobi.

"Afisi yetu iko tayari kugharamia nauli ya walimu walio na nia yakusafiri hadi Nairobi. Nawasihi wale walio na nia hiyo kujisajili kwenye afisi za chama hiki huko Keroka,” aliongezea Oteki.