Walimu wa shule za msingi katika kaunti ya Nyamira wameombwa kushirikiana na wahudumu wa afya kufanikisha chanjo ya ugonjwa wa ukambi na rubella kwa watoto, chanjo ambayo ilianza tarehe 16 Mai hadi 24 mwezi huu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mjini Nyamira siku ya Jumatatu,  daktari mkuu katika kaunti ya Nyamira Jack Magara alisema kuwa wanafunzi wote walio chini ya miaka 14 wanafaa kupata chanjo hiyo, na kuomba ushirikiano wa walimu kuhakikisha wamepata chanjo hiyo.

“Kuanzia leo wahudumu wa afya watatembea kwa mashule mbalimbali,  naomba walimu washirikiane nao ili kufanikisha chanjo hiyo katika kaunti hiyo,” alisema Jack Magara.

Wakati huo huo, Magara alisema kuwa ugonjwa wa ukambi hauponi ila kuchanjwa mapema ili watoto kutoathirika.

“Uchunguzi unaonyesha ugonjwa wa ukambi, ni mbaya sana ukianza kuathirika hauponi naomba kila mzazi kuhakikisha mtoto wake aliye na miezi tisa hadi miaka 14 kuhakikisha amechanjwa dhidi ya ugonjwa huo wa ukambi,” aliongeza Magara.