Walinzi wa kampuni ya Solvit Securty Guards walipofikishwa kizimbani. [Picha. Radiorahma.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Walinzi wawili wa kampuni ya Solvit Security guards wamekanusha mashtaka ya mauaji ya aliyekuwa mfanyikazi wa benki ya Stanbic.Hamisi Karisa na Said Mwalungo wanadaiwa kumuua David Kamau katika eneo la Nyali Centre mnamo Januari 7, mwaka huu.Washukiwa hao watazuiliwa kwa muda wa wiki moja hadi pale afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa itakabidhiwa ripoti ya upelelezi kutoka kwa maafisa wanaochuguza kesi hiyo.Hii ni baada ya mwendesha mashtaka Erick Masila kuomba muda huo ili aweze kujitayarisha kupinga kuachiliwa kwa dhamana kwa washukiwa hao.Masilia alisema kuwa hajapata ripoti kamili ya uchunguzi kutoka kwa maafisa wanaochunguza kesi hiyo.Kauli hii inajiri baada ya wakili wa washukiwa hao Cherie Oyier kuomba wateja wake kuachiliwa kwa dhamana.Akizungumza mbele ya jaji Dora Chepkwonyi, wakili huyo alisema kuwa katiba inaruhusu kila mshukiwa kupewa dhamana ili kuwa huru hadi atakapopatikana na hatia.Na kwa upande wake, wakili Leonard Shimaka anayewakilisha familia ya mwendazake David Kamau ametaka kutiwa mbaroni kwa walinzi wengine saba ambao wanadaiwa kuhusika katika mauaji hayo.“Walinzi walikuwa tisa lakini hadi sasa waliokamatwa ni wawili pekee,” alisema Shimaka."Tunaomba polisi waweze kuwakamata waliosalia na wawafikishe mahakamani,” aliongeza Shimaka.Aidha, alidai kuwa walinzi hao ambao bado hawajakamatwa wameanza kutishia familia ya mwendazake.Shimaka vilevile amepinga kuachiliwa kwa dhamana kwa washukiwa hao kwa kusema kuwa huenda wakawatishia mashahidi wa kesi hiyo.Kesi hiyo itatajwa Februari 8, 2018.

Kuwa wa kwanza kujua kuhusiana na habari muhimu pindi zinapotokea. Tuma ujumbe kupitia nambari ya WhatsApp 0740950002 ukianza na mojawapo ya maneno yafuatayo ili uanze kupokea taarifa moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi: Mombasa Crime, Mombasa Politics, Mombasa Sports, Mombasa Agriculture, Mombasa Random, Mombasa Health, Mombasa Business, Mombasa Environment, Mombasa Entertainment, Mombasa Transport, Mombasa Opinion, Mombasa Education.