Walinzi wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi.
Wawili hao, Syleter Omondi na Peter Momanyi wanadaiwa kuiba 'drum' zaidi ya 600 za 'bitumen' mali ya Speeddag Interfreight katika eneo la Changamwe.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutekeleza wizi huo siku tofauti kati ya tarehe 18 na 20 mwezi Machi.
Wawili hao walikana shtaka hilo la wizi ya mali hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne mbele ya Hakimu Susan Shitub siku ya Jumanne.
Hakimu Shitubi aliagizia washukiwa hao waachiliwe kwa dhamana ya shilingi milioni mbili.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 11 mwezi Mei.