Share news tips with us here at Hivisasa

Walio na azma ya kuwania uwakilishi wa wadi ya Kisii ya kati eneo bunge la Nyaribari Chache wameombwa kutotumia mazishi kujipigia debe, huku wakiwaharibia walio mamlakani jina.

Akiongea siku ya Ijuumaa katika hafla ya mazishi katika Kijiji cha Bogiakumu, wadi ya Kisii ya kati, mwakilishi wa wadi hiyo Fred Monyenye aliwaomba walio azma ya kuwania kutotumia mazishi kujipiga kampeni kwa kuwalaumu viongozi walio mamlakani kwa sasa.

Aidha, alisema kuwa huu si wakati wa kampeini, bali ni wakati wa kufanya maendeleo katika wadi hiyo ili kuhakikisha kuwa hatua ya maendeleo imefikiwa.

Monyenye aliwakashfu wanasiasa hao kwa kumkosoa kila wakati katika wadi hiyo kwa msingi wa kugawanya wakaazi.

“Wakati huu si wa siasa, wakati ukifika siasa tutafanya, lakini kwa sasa tufanye maendeleo kwani hiyo ndio jambo la mhimu wakati huu na kuhakikisha kuwa maendeleo yamefikiwa,” alihoji Monyenye.

Wakaazi hao walisema kuwa maendeleo katika wadi hiyo yamepiga hatua kwani kuna barabara nyingi ambazo kwa sasa zimekarabatiwa na wanasherekea matunda ya ugatuzi.

“Monyenye amejaribu kwani mtu hawezi kufanya yote kwa wakati mmoja, na nitumai anaendelea kufanya mengi ya kutusaidia sisi kama wakazi, nampongeza kwa yale anayoendelea kutenda,” alihoji Benson Nyabiuto, mkazi.