Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho ameshikilia kuwa walioasi chama cha ODM na kujitanga kuunga mkono chama cha Jubilee lazima wajiuzulu mara moja kwani hawawezi kuwa katika vyama viwili kwa mujibu wa katiba ya nchini na mkataba wa chama.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wakaazi wa Kisauni mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Joho amesema kuwa chama cha ODM kamwe hakiwezi ruhusu kiongozi kutanga kujiunga na chama kingine na ilhali yeye bado yuko ndani ya chama cha ODM huku akisema kuwa vinara wa chama hicho watawatimua viongozi hao iwapo watakaidi kujiuzulu kwenye chama cha ODM kwani wanaziba nafasi za wafuasi wapya wanataka kujiunga na chama cha ODM.

Gavana Joho amesema kuwa mkataba wa chama hicho uko wazi kwa viongozi wanaolenga kuhama na kujiunga na vyama vingine na chama cha ODM bado kitasalia kuwa na wafuasi kwa maana ni chama cha Wakenya wote na kila kiongozi anayelenga kujiunga na chama hicho anaruhusiwa.

"Kuna viongozi wengine wako ODM na wanaonekana wakishirikiana na Jubilee sisi tunasema kuwa mkataba wa cha unaeleza wazi kuwa wajiuzulu na tufanye uchaguzi mwengine , hatutaki mtu yuko na sisi na anatusaliti hiyo sisi hatutaruhusu," alisema Joho.

Akionekana kugusia swala la vinara wa Cord kuhitilafiana kuhusu swala la kuchaguliwa kama rais kupitia mrengo huo, Joho amesema kuwa utaratibi wa mkataba utafatiwa na suluhisho litapatikana huku akiwataka wakaazi wa Mombasa na Wakenya kwa jumla kuondoa hofu kwani vinara hao wa Cord hawawezi kutengana.

"Wananchi wale vinara watu wa Cord wakiongozwa na Raila Amollo Odinga kamwe hawawezi kutengana kwa sababu wanapenda Wakenya na kuwafanyia maendeleo na wale wanaosema ati Cord itavunjika watangoja sana," aliongeza Joho.