Watu wachache walijitokeza katika usajili wa makurutu wa polisi Mvita leo asubuhi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Takriban wanaume mia mbili na wasichana wachache wamejitokeza katika usajili huwo kukiwemo na mchanganyiko wa waliotoka shule moja kwa moja na wale ambao wametoka kwenye vyuo na wale ambao wametoka kwenye huduma kwa taifa NYS.

Nasra Mohamed aliyejitokeza katika usajili huo amevunjika moyo baada ya kunyimwa nafasi kwa kuwa hakuwa na alama inayotarajiwa ya D + na nakuendelea. Alisema hii ni mara yake ya tatu kujaribu kuingia katika kikosi cha polisi lakini hajawahi kufaulu jambo ambalo limemvunja moyo.

Amelalama kuwa aliarifiwa vijana waliokuwa katika mradi wa kazi kwa vijana ndio watakaopewa kipaumbele lakini hilo halikuwa kama alivyokuwa amearifiwa awali.

Katika uwanja wa Khadija eneo bunge la Kisauni David Kileni ni mmoja wa vijana ambaye alihudumu katika huduma ya vijana NYS kwa muda wa miaka miwili lakini hakubahatika.

Na kuwaomba wakaazi wa eneo hilo wasife moyo na waendelee kujituma na watafanikiwa kimaisha.

Hata hivyo amewarai kuwa kukosa kazi leo isiwe sababu ya hao kuanza kujishughulisha na utovu wa usalama ama kuanza kubugia mihadarati.