Wanafunzi wa Taasisi ya Gusii Institute of Technology walizua rabsha tena hapo jana (Jumatano) muda mfupi tu baada ya Maafisa wa Polisi kuwahakikishia kuwa uchunguzi kabambe bado unaendelea.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya Afisa wa uchungunzi Moses Dindi pamoja na mwenyekiti wa kitengo cha Trafiki Joshua Mtakai kutembele mji wa Kisii Jumatano na kuwahakikishia wanafunzi hao na wakaazi wa Kaunti ya Kisii kuwa uchungunzi unaendelea kufanywa kuhusu rabsha zilizozuka katika mji huo ambapo Askari wa GSU alifyatulia risasi dereva mmoja na kufariki.

Wanafunzi hao walianza kuzua rabsha baada ya baadhi ya Askari kujaribu kuchukua vikingi vya stima vilivyobaki mahala gari hilo lilichomwa huku wakisema wanahitaji waliopoteza maisha yao kufuatia ajali hiyo kufidiwa kwanza.

Afisa anayesimamia Maafisa katika eneo la Nyanza Willy Lugusa alisema uchungunzi unaendelea kufanywa dhidi ya madai kuwa Afisa wa Polisi alikuwa akiendesha gari lililosababisha ajali na kuwahakikishia kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa pindi uchungunzi utakapomalizika.

Akizungumza Jumatano na Wandishi wa Habari katika Kituo cha Polisi cha Kisii Central, Lugusa alisema uchunguzi utafanywa kwa kina ili uwazi uonekane kwa wakaazi, wanafunzi na Wandisha wa Habari.

Wakati uo huo, Lugusa alikiri kuwa alikuwa na ziara tofauti katika mji wa Kisii bali si kuongea kuhusu ghasia zilizotokea katika mji wa Kisii huku akisema kuwa alikuja akitafuta suluhu jinsi Polisi kwa changamoto mbali mbali wanaopitia Maafisa wa eneo hilo.

Kwa upande mwingine wakaazi wa Kaunti hiyo wanamtaka Afisa wa Polisi aliyemfyatulia risasi dereva mmoja wa gari la Mizizi na kufariki papo hapo achukuliwe hatua mara moja huku wengi wakiwa madereva wa kituo cha magari ya kuelekea eneo la Keroka.

“Afisa yule aliyempiga risasi dereva mwezetu achukuliwe hatua la sivyo ni kama tunadhhulumiwa sisi wananchi wa kawaida,” alihoji Elijah Masega dereva wa magari ya kuelekea Keroka Sotik.