Jamii ya wamakonde.[Picha/jamiiforums.com]
Jamii ya wa Makonde kwa mara ya kwanza wameadhimisha siku ya Jamuhuri nchini Tangu kutambuliwa kwao kama wakenya.
Akizungumza katika sherehe za Jamuhuri huko Kinondo eneo la Msambweni Wameipongeza serikali ya Jubilee kwa kuwatambua kama wakenya halisi.
Wakiongozwa na Thomas Nguli ambaye ni mwenyekiti wa jamii ya wa Makonde,alisema kuwa wanajivunia kuwa wakenya na wataendelea kuunga mkono serikali ya Jubilee.
“Tunajivunia kuwa wakenya,tutazidi kupongeza serikali bila kinyongo”,alisema Nguli.
Nguli amezitaka jamii zingine kukubali wamakonde kama wakenya kwani bado wadhalilishwa na baadhi ya watu licha ya kutambuliwa na serikali.
“sisi pia ni wakenya, jamii zingine zinafaa kutujali bila kutubagua‘,alisema Nguli.
Aidha ameitaka serikali kuwajumuisha wakomande katika shughuli za kimaendeleo na mipango yake serikali ili nao kujihisi kama wakenya wengine.
“Tunataka kujumuishwa kwenye miradi ya maendeleo na sisi tufaidike kama wakenya‘,alisema Nguli.