Waziri wa maji nchini Eugene Wamalwa ametoa wito kwa viongozi katika kanda ya Pwani kutofautisha mambo ya maendeleo na siasa za vyama.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea katika mkutano ya washika dau katika sekta ya maji kanda ya Pwani ulioandaliwa katika hoteli ya Pride Inn mjini Mombasa siku ya ijumaa, waziri huyo alisema kuwa ni haki ya kila Mkenya kupata maji safi licha ya chama cha kisiasa anachoshabikia.

Waziri huyo alitoa makataa ya siku 21 kwa bodi ya maji katika kanda ya Pwani kuanza miradi za usambazaji maji safi katika eneo ya Malindi, ambalo limekuwa likikumbwa na changamoto ya uhaba wa maji mara kwa mara.

Aidha, mbunge wa Malindi Willy Mtengo alikaribisha amri hiyo kwa kusema kuwa eneo bunge hilo lina miradi ya maji ambayo haijakamilishwa kwa miaka mingi, na kuitaka serikali kuingilia kati na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa.