Watu wanaomiliki mbwa katika mtaa wa Maili Sita huko Bahati wametakiwa kuwafungia mbwa wao haswa nyakati za mchana.

Share news tips with us here at Hivisasa

Agizo hilo limetolewa an chifu wa eneo hilo Daniel Maina baada ya wanafunzi watatu kuumwa na mbwa walipokuwa wakitoka shuleni hapo siju ya Ijumaa katika visa viwili tofauti.

Chifu Maina aliwataka wamiliki wa mbwa kuwafungia mbwa hao na kuonya kuwa mbwa atakaye patikana akirandaranda atakamatwa na kukabidhiwa maafisa wa afya idara ya mifugo katika Kaunti ya Nakuru.

Akiongea katika soko la Maili Sita Jumamosi asubuhi alipowahutubia wakaazi, Maina alisikitikia ongezeko la mbwa hao wa kurandaranda na kuwataka wanafunzi kuwa waangalifu sana na kutemeba katika makundi haswa nyakati za mchana wanapotoka shuleni.

“Kuna mbwa wengi sana ambao wanazurura katika kijiji hiki na juzi kuna watoto watatu hapa Kiamaina wameumwa na mbwa walipokuwa wakitoka shuleni na ningependa kusema kuwa iwapo wenye mbwa hao hawatawafungia mbwa wao kwa sababu maisha ya watoto wetu hayawezi kuhatarishwa na wachache,” alisema chifu Maina.

Mina pia aliwataka waliofuga mbwa kuhakikisha kuwa mbwa wao wamepewa chanjo cha ugonjwa wa kichaa cha umbwa ili kuwakinga sio hao tu, bali raia pia.