Wamiliki wa majumba ya kukodi katika Kaunti ya Kisumu wametakiwa kuhakikisha kuwa wanawasambazia wakaazi maji safi ya mfereji.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumamosi, afisa mshirikishi wa uchunguzi wa magonjwa katika Kaunti ya Kisumu Dkt Elly Nyambok alisema kuwa ni muhimu kwa wadau wote kuchangia katikakuimarisha huduma za maji safi.

Alitoa wito kwa wachuuzi wa maji mitaani kuhakikisha kuwa wanateka na kuwauzia wakaazi maji safi.

Aidha, aliwashauri wakaazi wanaonunua maji hayo, kuwashinikiza wachuuzi hao kuzingatia usafi ikiwemo kuwataka kuosha vizuri vibuyu wanavyotumia kubebea maji hayo.

Nyambok pia aliwahimiza wakaazi kutowapeleka mifugo wao mitoni kunywa maji, kwa kusema kuwa hatua hiyo hupelekea mifugo hao kuchafua maji kwa kuenda haja, hali inayo hatarisha afya wa wakaazi wanaotumia maji ya mto.

''Wanaopeleka ng'ombe, mbuzi na mifugo wengine mitoni kunywa maji inafaa wabuni mbinu mbadala ya kuwapa mifugo hao maji kwa maana wanapoenda mtoni, hao huishia kuharibu mazingira kwa kuweka samadi na mkojo,” alisema Dkt Nyambok.