Wakaazi wa eneo la Mwachamago huko Likoni, wamewataka wamiliki wa nyumba katika eneo hilo kuwawajibika katika uchimbaji wa majaa ya taka ili kusaidia katika udumishaji wa mazingira safi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yamejiri wakati ambapo wapangaji wa nyumba katika sehemu hizo wameonekana kutupa taka kiholela, bila kuzingatia madhara ya baadaye.

Solomon Atuti, mkaazi Mwachamago, alieleza kugadhabishwa mno na tabia hiyo huku akisema kuwa huenda kukazuka mkurupuko kwa magonjwa ifikapo msimu wa mvua nyingi.

Ali Maneno, mkaazi, aliunga matamshi ya Achoki mkono na kuwaomba wapangaji kubuni mbinu ya kutupa taka mahali pamoja na kisha kuzichoma kama njia mojawapo ya kuzipunguza.

Aisha Mbwana, kwa upande wake, aliilaumu serikali ya kaunti kwa kutowatengea majaa ya taka katika eneo hilo.