Wakaaji wa mji wa Kisii na vitongoji vyake wameombwa kutunza mazingira mahala wanamoishi, ili kuepuka maradhi ya kila mara na kujikinga na vyakula ambavyo vinapikwa mahala palipo wazi ili kuepukana na na mukurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao imekita mizizi katika Kaunti ya Migori na katika mpaka wa kaunti ya Kisii.
Akiongea siku ya Jumatano, mama Roseline Motanu mmiliki wa katika sehemu ya Gekomu Kaunti ya Kisii amesema wapangaji wanastahili kudumisha usafi ili kuendelea kuishi katika mazingira safi.
“Wapangaji wengi huwa hawazingatii usafi, wakati mwingi hufikiria hiyo ni kazi ya mwenye nyumba ambapo ni kinyume,” alisema Motanu.
Kwingineko kutokana na kupanuliwa na kufunguliwa kwa baadhi za barabara katika Kaunti ya Kisii, wamiliki wa nyumba katika mji huo wamesema ni mojawapo ya njia ya kuwarahisishia kazi wapangaji wa nyumba hizo kwa kuzifikia kwa haraka.
Aidha, amewaomba wamiliki wa nyumba Katika kaunti hiy kuungana pamoja na kuunda chama kimoja ambacho kitaweza kuwasaidia katika siku zijazo.
Kwa upande mwingine, wapangaji, hasa katika mtaa wa mwembe mji wa Kisii wamewaomba wanaomiliki nyumba katika mji huo kuwahakikishia usalama wa kutosha, wakilalamikia kwamba wanapotoka kazini, hushtukia milango ya nyumba zao imevunjwa na wezi na baadaye kupata mali yao imeporwa.